Wednesday, 17 August 2016

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange afariki dunia

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.Mbrazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.
Alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA April 2013 kufuatia uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa,na kulazwa
hospitalini mwaka uliofuata alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.
Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.
Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936,mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.
Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.

Tuesday, 16 August 2016

Conte awa kuvutio

Kocha wa Chelsea Antonio Conte awa kivutio katika game ya kwanza ya Premier league .
Chelsea ilifanikiwa kuwafunga wangonga nyundo wa London kwa goli 2 kwa 1.
Hazard kwa penalty na Costa dk.89.
Hivyo na kufanya makocha wapya wote kuanza  kwa ushindi.

Rio 2016: Usain ashinda dhahabu ya mita mia 100 akifuatwa na Justin Gatlin

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya olimpiki ya Rio 2016.
Bolt, 29, amechukua muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.
Gatlin, ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.
"Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda," Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake.
Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.
Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa dunia mwaka 2017.

Homa ya manjano ni tishio ulimwenguni

Shirika la kimataifa la Save the Children limetahadharisha kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano katika nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola kuwa hivi karibuni unaweza kuenea katika nchi za mabara ya ulaya , Amerika na Asia.
Ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya aedes, wanaopatikana katika nchi nyingi za Afrika Magharibi.
Mlipuko wa ugonjwa huo barani unaelezwa kuwa mkubwa kuliko miaka 30 iliyopita na umesababisha kutumika kwa chanjo mara nne kuliko ilivyo kawaida kwa mwaka huu pekee jambo lililofanya Shrika la Afya duniani WHO kupunguza kiwango cha dozi ili kuwezesha watu wengi zaidi kupata chanjo hiyo.
Shirika hilo la Save the children limesema limetuma wataalamu wake kusaidiana na serikali ya DRC kutoa chanjo homa hiyo ya manjano kwa watu nusu milioni katika mji mkuu wa Kinshasa.
Tayari mzungumko wa kwanza wa chanjo hiyo ilishatolewa katika mji huo wa Kinshasa baada ya kuthibitishwa kulipuka kwa ugonjwa huo ambao hauna tiba.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa katika nchi jirani ya Angola kabla ya kuenea nchi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Zaidi ya watu mia nne walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika nchi hizo mbili ambapo huku wengine zaidi ya watu elfu sita wakiripotiwa kuambukiza ugonjwa huo.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema hakuna maambukizi mapya yaliyoripotiwa nchini Angola tangu mwezi juni , na kufufua matumaini kwamba ugonjwa huo sasa utadhibitiwa.

Mtoto Zephany Nurse aibwa hospitali Afrika Kusini

Mahakama moja nchini Afrika Kusini imemhukumu mwanamke mmoja kifungo cha miaka kumi jela kwa kosa la kumteka nyara mtoto mchanga yapata miaka ishirini iliyopita na kumkuza huku akimuamisha kuwa yeye ndiye mama yake mzazi.
Mwanamke huyo sasa ana umri wa miaka hamsini amekana madai ya yanayomkabili ya udanganyifu na utekaji nyara.Muuguzi Zephany anasema mtoto huyo mchanga alinyakuliwa alipokuwa amelala kwenye kitanda kando y mama yake katika hospitali iliyoko mjini Cape Town.
Tuhuma dhidi ya mwanamke huyo zilianza tangu mnamo mwaka jana mara baada ya binti aliye mwiba kuanzisha urafiki baina yake na msichana mdogo aliyekuwa anasoma naye kufanana mpaka kutia fora.Uchunguzi wa vinasaba ulipofanywa, watoto hao waligundulika kuwa ni ndugu.
Hakimu Hlope alimwambia mshtakiwa kwamba ameidanganya mahakama yake na haonekani kujutia kosa lake.

Aboud Jumbe aaga dunia kigamboni jijini

Rais mstaafu wa awamu ya pili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia Jumapili saa saba mchana nyumbani kwake katika kijiji cha Mji Mwema, eneo la kigamboni jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bwana Mohamed Aboud, mwili wa Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye pia alikuwa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unatarajiwa kusafirishwa Jumatatu kwa ndege kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya maziko.
Bwana Mohamed Aboud amesema Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake eneo la Migombani, Mkoa wa Mjini Maghrib mnamo saa saba za mchana. Marehemu amefariki akiwa na umri wa miaka 96 alizaliwa June 14, 1920 huko Juba, Sudan Kusini.
Aidha viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanatarajia kuhudhuria maziko hayo ya Marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi .
Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi alishika wadhifa wa Rais wa Zanzibar April 7, 1972 mara tu baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa kwanza wa visiwa hivyo Abeid Amani Karume. Hayati Aboud Jumbe alijiuzulu urais wa Zanzibar pamoja na nyadhifa nyingine za makamu mwenyekiti wa CCM na makamu rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Januari 30, 1984.
Mungu alizale roho ya Marehemu mahali pema peponi

Monday, 8 August 2016

"NINA UHAKIKA NA UBINGWA MSIMU UJAO"- GEOFREY NYANGE 'KABURU'

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kujiandaa na Ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu ujao.
Kaburu ameiambia Goal kwamba mabadiliko ya kikosi walichosajili kwa ajili ya msimu ujao ndivyo vinavyo wapa matumaini ya kubeba taji hilo msimu ujao.
"Mabadiliko yetu hayapo kwenye uongozi bali hata usajili wetu wa msimu ujao umetulia tumesajili vizuri na ninauhakika na ubingwa msimu ujao" amesema kaburu.
Simba ambayo msimu ujao itakuwa chini ya kocha Mcameroon Joseph Omog jana ilikamilisha usajili wake wa msimu ujao akiwemo mchezaji Lodit Mavugo aliyetokea Vital'o ya Burundi.

JOSE MOURINHO: "HATIMAYE TUMEMPATA PAUL POGBA"

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amekiri kuwa "hatimaye" klabu yake imefanikiwa kuipata huduma ya Paul Pogba kutoka Juventus
Mustakabali wa Pogba ulikuwa umezungukwa na tetesi nyingi mno majuma ya hivi karibuni, kwa nyota huyo kusajiliwa kwa ada ya kuvunja rekodi na Mashetani Wekundu.
Uthibitisho rasmi ulipatikana leo kutoka klabuni hapo kwamba Mfaransa huyo amepewa ruhusa na Juventus kuendelea na vipimo Manchester, lakini Mourinho ameonya kuwa hana uhakika wa namba katika kikosi chake.
"Pogba? Hatimaye, ni mchezaji mahiri. Mchezaji mzuri kama yeye atakuwa pamoja nasi, hatimaye tunaye," alisema Mourinho.
"Hatimaye tunaye. Anaungana na kikosi cha ushindi. Lakini atalazimika kufanya bidii nyingi kuingia kwenye kikosi. United ni klabu sahihi ambayo itamweka kwenye viwango anavyohitaji kuwa.
"Nimemwona Pogba akikimbia, akicheza kikapu, hufanya kila kitu, kwahiyo natumai atakuwa fiti. Nitakuwa nikimsubiri Jumanne."
Mourinho amenyanyua taji lake la kwanza kama meneja wa United kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City katika mechi ya Ngao ya Jamii iliyopigwa Wembley Jumapili mchana.

Oscar Pistorius ajeruhiwa gerezani

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani anakohudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuuwa mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp.
Kuna ripoti inayosema kuwa alikuwa amejeruhiwa kwenye kifundo cha mkono.
Kumeibuku uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.
Mwezi uliopita, waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa watakata rufaa kupinga hukumu ya miaka sita ya Pistorius, wakisema kuwa ni hukumu ndogo mno.
Mwanariadha huyo alimuuwa mpenziwe wa kike , kwa kumpiga risasi nyumbani kwake wakati wa siku kuu ya wapendanao mnamo mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi.

Sakata la Yanga

Nafurahi kuona Tanzania inafufuka katika sokaa!!
Natamani kuona kila pedeshyeeee akimiliki timu moja ya ligi juu na kujenga kiwanja maendeleo ya timu yasonge mbele!!!
Yanga na sakata lao muwaaachie wenyewe ,majibu mtayapata baaada ya miaka 4 ,natumai wengine mtajifunza hapo

Pogback

Pogba ameshatua London na ameshafanyiwa vipimo Leo kutangazwa rasmiii!!