“Ni lazma Yanga watambue wanaliwakilisha Taifa” – Jamal Malinzi
Kikosi cha timu ya Yanga kinaondoka kesho kikiwa na
matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya ushindi wa mabao 5-1
iliyoupata kwenye mchezo wa awali
WAKATI kikosi cha Yanga kikiondoka nchini kesho kuelekea Harare
Zimbabwe Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi
amewatahadharisha wawakilishi hao pekee wa Tanzania kwenye michuano ya
Kombe la Shirikisho kwa kuwataka wacheze kwa jihadi ili wasonge mbele.Malinzi ameiambia Goal, FC Platinum inauwezo mkubwa hivyo nilazima wachezaji wa Yanga watambue kama wanaliwakilisha taifa hivyo wanachotakiwa ni kucheza kwa bidii bila kuangalia matokeo ya mechi ya kwanza waliyoshinda mabao 5-1, lengo likiwa ni kusonga kupata ushindi wa mapema utakao wachanganya wapinzani wao na kusonga mbele.
“Nimezungumza na nahodha wa Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ nimemwambia awaeleze wenzake taifa linawatazama wao hivyo wanatakiwa kucheza kwa tahadhari na kujituma ili wapate ushindi wakiwa ugenini. Kwani Platinum ni timu ngumu na wanacheza nyumbani kwao uwezekano wa kupata mabao matano upo kama vile wao walivyopata wakiwa nyumbani,”amesema Malinzi.
Kikosi cha timu ya Yanga kinaondoka kesho kikiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya ushindi wa mabao 5-1 iliyoupata kwenye mchezo wa awali na kocha Pluijm amesema watakwenda kushambulia kama walivyofanya nyumbani na siyo kuzuia kama zinavyofanya baadhi ya timu.
YANGA DAIMA MBELENYUMA MWIKO
ReplyDelete