Wednesday, 25 October 2017

Friday, 2 September 2016

Wanajimu katika maeneo tofauti ya bara Afrika wameona moto wa mviringo angani wakati wa kupatwa kwa jua.

Jua hupatwa wakati ambapo mwezi huwa mbali na dunia ikilinganishwa na wakati jua linapopatwa kabisa.
Matokeo yake huwa ni mviringo mkubwa unaong'aa ukiwa umezunguka eneo jeusi .
Picha nzuri ni zile zilizoonekana nchini Tanzania ambapo tukio hilo lilichukua mda wa dakika tatu.
Kupatwa huko kwa jua pia kulionekana nchini Gabon,Congo-Brazaville,DRC Madagascar na kisiwa cha Re-union.
Wakati ambapo mwezi uko mbali na dunia ,huonekana mdogo na hauwezi kuliziba jua kabisa wakati wa kupatwa kwa jua.Matokeo yake hujulikana kama mviringo wa moto.
Kupatwa kwengine kwa jua kunatarajiwa kufanyika mnamo mwezi Februari 2017 na huenda kukaonekana katika maeneo ya Marekani kusini na Africa.

Mwanzilishi wa kampuni ya facebook Mark Zuckerberg amezuru nchini Kenya katika ziara yake ya mataifa ya bara Afrika.

Zuckerberg aliyewasili siku ya Jumatano kutoka nchini Nigeria alifanya kikao na waziri wa habari nchini Kenya Joseph Mucheru,ambapo walizungumza kuhusu mtandao na mipango ya serikali kuhakikisha kila kijiji kimeunganishwa na mtandao.
Baadaye Zuckerbag aliekea katika hoteli ya Mama Oliech katika chakula cha mchana ambapo kwa mara ya kwanza alikula Ugali na Samaki.
''Swala muhimu ninapozuru taifa lolote jipya ni kujaribu kula chakula chao.Nilipenda sana ugali na samaki mzima wa tilapia'',alisema Zuckerberg.

Wednesday, 17 August 2016

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange afariki dunia

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.Mbrazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.
Alijiuzulu nafasi ya Urais wa FIFA April 2013 kufuatia uchunguzi wa madai ya kupokea rushwa,na kulazwa
hospitalini mwaka uliofuata alipokumbwa na ugonjwa wa mapafu.
Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.
Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936,mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.
Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.

Tuesday, 16 August 2016

Conte awa kuvutio

Kocha wa Chelsea Antonio Conte awa kivutio katika game ya kwanza ya Premier league .
Chelsea ilifanikiwa kuwafunga wangonga nyundo wa London kwa goli 2 kwa 1.
Hazard kwa penalty na Costa dk.89.
Hivyo na kufanya makocha wapya wote kuanza  kwa ushindi.

Rio 2016: Usain ashinda dhahabu ya mita mia 100 akifuatwa na Justin Gatlin

Mwanariadha wa Jamaica, Usain Bolt, ameandikisha historia ya kuwa mwanariadha wa kwanza kushinda nishani ya dhahabu kwa mara ya tatu mfululizo, katika mbio za mita mia moja, kwenye michezo ya olimpiki ya Rio 2016.
Bolt, 29, amechukua muda wa sekunde 9.81 katika fainali yake ya mwisho katika michezo ya olimpiki, kwa kuiga ushindi sawa na huo katika michezo ya olimpiki mjini Beijing 2008, na London 2012.
Gatlin, ambaye amepigwa marufuku mara mbili kwa matumizi ya dawa za kutitimua misuli, alimaliza sekunde 0.08 nyumna ya Bolt na kuchukua nishani ya fedha.
"Nilitarajia kwenda kasi zaidi, lakini nafurahia kwamba nimeshinda," Bolt ameiambia BBC.
Mwanariadha wa Canada Andre de Grasse ameshinda nishani ya shaba, na kuandikisha muda bora wa kibinafsi wa sekunde 9.91, mbele ya mwanariadha wa Jamaica Yohan Blake.
Bolt anatazamia kuondoka Rio na nishani zaidi za dhahabu katika mbio za mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti, jinsi ilivyokuwa katika michezo ya olimpiki ya mwaka 2008 na 2012.
Mwanariadha huyo anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 alisema kuwa atastaafu kutoka kwenye ulingo wa riadha baada ya michuano ya ubingwa dunia mwaka 2017.

Homa ya manjano ni tishio ulimwenguni

Shirika la kimataifa la Save the Children limetahadharisha kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa homa ya manjano katika nchi za Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Angola kuwa hivi karibuni unaweza kuenea katika nchi za mabara ya ulaya , Amerika na Asia.
Ugonjwa huo unaenezwa na mbu aina ya aedes, wanaopatikana katika nchi nyingi za Afrika Magharibi.
Mlipuko wa ugonjwa huo barani unaelezwa kuwa mkubwa kuliko miaka 30 iliyopita na umesababisha kutumika kwa chanjo mara nne kuliko ilivyo kawaida kwa mwaka huu pekee jambo lililofanya Shrika la Afya duniani WHO kupunguza kiwango cha dozi ili kuwezesha watu wengi zaidi kupata chanjo hiyo.
Shirika hilo la Save the children limesema limetuma wataalamu wake kusaidiana na serikali ya DRC kutoa chanjo homa hiyo ya manjano kwa watu nusu milioni katika mji mkuu wa Kinshasa.
Tayari mzungumko wa kwanza wa chanjo hiyo ilishatolewa katika mji huo wa Kinshasa baada ya kuthibitishwa kulipuka kwa ugonjwa huo ambao hauna tiba.
Awali ugonjwa huo uliripotiwa katika nchi jirani ya Angola kabla ya kuenea nchi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Zaidi ya watu mia nne walioambukizwa ugonjwa huo wamefariki katika nchi hizo mbili ambapo huku wengine zaidi ya watu elfu sita wakiripotiwa kuambukiza ugonjwa huo.
Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema hakuna maambukizi mapya yaliyoripotiwa nchini Angola tangu mwezi juni , na kufufua matumaini kwamba ugonjwa huo sasa utadhibitiwa.